welcome

dear viewers... karibuni katika blog yetu. kwa mawasiliano zaidi utatupata kwa email nicarwag@gmail.com. simu 0758921901

Saturday, July 9, 2011

JUA ISHARA TANO ZA MWANAMKE ANAETAKA KUDATE NA WEWE


 KUCHEKA
Hii ni ishara nzuri sana. kwa mwanamke kupenda kucheka mbele ya mwanaume anaetamani ku date nae. Humfanya mwanaume kama comedian fulani kwa kucheka kila anpomuona hata kama hata haujakaa kuchekesha kihivo. Na hata wanawake wengi huvutiwa hasa na mwanaume ambaye anakuwa funy kwake na kumfanya acheke katika kipindi cha kutongozana.
MUDA WA KUPIGA STORY
Kama unarafiki wa jinsia ya kike angaliane wakati na mahali ambapo yeye anataka mtoke. Kama anataka kukutana na wewe kwa ajili ya chakula cha mchana na mida ya mchana ujue hajavutiwa ku date na wewe ila kama atataka mkutane mida ya jioni na usiku au akakuomba kwenda kuangalia movie mida ya usiku jua amevutiwa na wewe huyo.
VIUNGO VYA MWILI KUONGEA.
Lugha ya mwili ni ishara mojawapo ya kumtambua mwanamke anaempenda mwanaume. Mnaweza kuwa mpo nje na akaanza kukushika shika mikono yako wakati hamna utani wa aina hiyo kati yenu wakusema aweze kukushika mikono. Mwanamke hutumia sana vitendo katika kuexpress fellings zake, mwili wa mwanamke hutoa lugha mbalimbali zenye maana kubwa katika mapenzi kama vile kukuegemea wakati mnaongea hizi ni dalili nzuri.
MUONEKANO. “SHE LIKES YOU”
Unapaswa kuangalia eye contact.macho kwa macho kati yenu yakidumu kwa muda zaidi ya sekunde mbili ni ishara nzuri. Kama mwanamke atakuwa anaangalia  kuanzia machoni mwako mpaka mdomoni basi mambo hapo ni mazuri sana
CHUKUA HATUA
Mara nyingi wanaume wakishatambua kuwa mwanamke fulani anampenda  akili zao huwatumwa kuwa hawana even an idea on how to proceed. Unatakiwa uendelee baada ya yeye kukupa mwanga sio kuacha yeye aendelee. Muombe kuzungumza nae mbali na marafiki zake au kwa kupitia simu yake ya mkononi. Muombe kutoka nae dinner mkiwa wawili tu. Mwambie ungependa kuwa zaidi ya rafiki kwake na vingineo. Ama hakika jibu litakuwa ndiyo.

No comments: