welcome

dear viewers... karibuni katika blog yetu. kwa mawasiliano zaidi utatupata kwa email nicarwag@gmail.com. simu 0758921901

Monday, May 27, 2013

FEDHA KESSY NA NANDO WAIWAKILISHA TANZANIA KWENYE SHINDANO LA BIG BROTHER THE CHASE 2013.


IMG_0156
Kundi la Mafikizolo la nchini Afrika Kusini likitoa burudani wakati wa uzinduzi wa show ya Big Brother-The Chase iliyorushwa Live na Channel za DStv 197 na 198 jijini Johannesburg usiku huu. Shindano la Big Brother-The Chase limedhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel. (Picha na Dewji Blog)
IMG_0140
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo waandishi wa habari kutoka nchin mbalimbali za Afrika kushuhudia Live uzinduzi huo.
IMG_0209
Mwakilishi kutoka Tanzania Nando akihojiwa na Mtangazaji wa kipindi hicho Ik wakati wa uzinduzi wa show hiyo.Kushoto patna wa Nando Mshiriki kutoka Namibia Cleo.
IMG_0226
Mwakilishi wa Tanzania Fedha Kessy akiwasalimu mashabiki wake kwa kuwapungia bendera ya Tanzania. Kulia ni mtangazaji wa Shindano la Big Brother The Chase 2013 Ik.
IMG_0231
Mtangazaji IK akifanya mahojiano na Patna wa Mwakilishi wa Tanzania Mshiriki kutoka Ghana Elikem wakati wa uzinduzi wa Shindano la Big Brother The Chase lililozinduliwa rasmi leo jijini Johannesburg Afrika Kusini ambapo washiriki watakaa ndani ya jumba hilo kwa siku 90 na mshindi kujinyakulia kitita cha Usd 300,000. Kulia ni Fedha Kessy mshiriki kutoka Tanzania.
IMG_0235
Mtangazaji IK akimtambulisha rasmi mshiriki kutoka Tanzania Fedha Kessy kwa Patna wake Mshiriki kutoka Ghana Elikem wakati wa uzinduzi wa shindano hilo leo jijini Johannesburg.