jina Al-Shabab linamaanisha Kijana kwa lugha
ya kiarabu. Kundi hilo liliibuka kama tawi la vijana la muungano wa
mahakama za kiislmau ambao baadaye ulivunjika mwaka 2006, wakati
ilipopigana na wanajeshi wa Ethiopia waliokuwa wameingia nchini Somalia
kuunga mkono serikali iliyokuwa dhaifu.
Kundi hilo limeweka sheria kali za kiisilamu
katika maeneo ambayo linadhibiti ikiwemo kupigwa kwa mawe hadi kufa
wanawake wanaodaiwa kufanya uasherati pamoja na kuwakata wezi mikono.
Je Al Shabaab linadhibiti sehemu gani ya Somalia?
Ingawa kundi hilo limepoteza udhibiti, wa miji mikubwa, bado linakita mizizi katika maeneo ya mashinani.
Lililazimika kuondoka katika mji mkuu Mogadishu,
mwezi Agosti mwaka 2011 na pia kuondoka katika mji wa bandarini wa
Kismayo mwezi Septemba mwaka 2012.
Kismayo ulikuwa mji muhimu kwa kundi hilo, ambao
ulikuwa unawezesha bidhaa kuwafikia wapiganaji wa kundi hilo pamoja na
kuwatoza watu ushuru kwa shughuli zao.
Muungano wa Afrika, ambao unaunga mkono juhudi za majeshi ya
serikali, ulisherehekea ushindi huo ingawa al-Shabab hunfanya
mashambulizi ya mara kwa mara ya kujitoa mhanga mjini Mogadishu na
kwingineko.
Wadadisi wanaamini kuwa al-Shabab limeanza
kufanya mashambulizi ya kuvizia baada ya kushindwa na majeshi ya
Muungano wa Afrika wanaotumia nguvu dhidi yao.
Lakini linakabiliwa na tisho kubwa kutoka kwa wanajeshi wa Kenya walianza hatarakti zao dhidi ya kundi hilo kuanzia mwaka 2011.
Kenya ilituhumu wapiganaji wa al-Shabab kwa
kuwateka nyara wanajeshi wake pamoja na watalii na sasa wamekuwa katika
msitari wa mbele kupambana na kundi hilo la kigaidi.
Wakati huo, wanajeshi wa Ethiopia waliweza kukabiliana na wapiganaji hao na kudhibiti miji ya Beledweyne na Baidoa.
Nani kiongozi wa al-Shabab?
Ahmed Abdi Godane ndiye kiongozi wa kundi hilo. Anajulikana kama Mukhtar Abu Zubair, na anatoka katika jimbo la Somaliland.
Kumekuwa na taarifa za mgawanyiko katika kundi
hilo, ambazo hata hivyo zinapingwa vikali na kundi lenyewe. Inaarifiwa
kuwa uongozi wake unapingwa, na wanachama wanaotoka maeneo ya Kusini na
ambao ni wengi katika kundi hilo. Inakisiwa idadi yao ni kati ya
wanajeshi 7,000 na 9,000.
Bwana Godane huwa haonekani hadharani .
Mtangulizi wake Moalim Aden Hashi Ayro, aliuawa katika shambulizi
lililofanywa na Marekani mwaka 2008.
Nini uhusiano wa kimataifa wa kundi hilo?
Al-Shabab lilijiunga na al-Qaeda mwezi Februari
mwaka 2012. Katika ujumbe wa Video, kiongozi wa al-Shabab Ahmed Abdi
Godane alisema anaahidi kuunga mkono kingozi wa al-Qaeda Ayman
al-Zawahiri.
Makundi hayo mawili yamekuwa yakifanya kazi kwa
pamoja, na raia wa kigeni wamekuwa wakiunga mkono kundi hilo, na hata
kuwasaidia katika harakati zao za mapigano.
Mwaka jana maafisa wa al-Shabab waliambatana na
mtu aliyesema ni mwanachama wa al-Qaeda na kumtambua kuwa raia wa
Marekani Abu Abdulla Almuhajir alipokuwa anatoa msaada wa chakula kwa
waathiriwa wa njaa.
Maafisa nchini Marekani wanaamini kuwa
wapiganaji wa Al Qaeeda ambao hawajahusina sana na mashambulizi nchini
Afghanistan na Pakistan kufuatia mauaji ya kiongozi wao,Osama bin Laden,
wapiganaji wake wengi wanakwenda kutafuta hifadhi nchini Somalia.