welcome

dear viewers... karibuni katika blog yetu. kwa mawasiliano zaidi utatupata kwa email nicarwag@gmail.com. simu 0758921901

Saturday, February 21, 2015

Kuelekea Tuzo za Oscar tarehe 22 February.. Wanaharakati wacharuka




 
Baadhi ya makundi ya haki za kiraia nchini Marekani yamesema kuwa, Tunzo za Oscar za mwaka huu zime kosa utofauti baada ya waigizaji wote 20 walioteuliwa kuwa ni wazungu huku muigizaji katika filamu iliyofanya vizuri ya Selma akikosa uteuzi huo.

Wanaharakati hao wamesema kuwa wanapanga kuandama nje ukumbi siku ya Jumapili wakati wa sherehe za utoaji wa tuzo hizo.




SELMA Ni filamu ya kiharakati na haki za kiraia inayo muelezea Mwanaharakati Martin Luther King ijulikanayo kama Selma.

Pamoja na kufanya vizuri kwa sasa, muhusika mkuu katika filamu hii hakuweza kuteuliwa kabisa katika vipengele kama muigizaji bora.

Wadau wa burudani wanasema kuwa filamu ya selma imebeba ujumbe mzito kwa jamii na wanashangaa Muhusika mkuu kuto teuliwa katika vipengele vya Oscar.



Lengo la maandamano hayo ni kufikisha ujumbe kwa kamati ya Oscar, Hollywood na sekta ya filamu kwa ujumla



Kumekuwa na mijadala mbalimbali inayoendelea katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari tangu uteuzi wa tunzo hizo zilipo tangazwa.