Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries
Limited (TDL), David Mgwassa, akionesha kinywaji cha Afrika Kusini
kilichofungwa kwenye viroba kama ambavyo Konyagi inafanya hapa
nchini.Vinywaji kama hivyo vipo karibu nchi nyingi Ulimwenguni.
Meneja wa Masoko wa Konyagi, Joseph Chibehe akielezea jinsi vinywaji vyao vinavyochangia mapato ta serikali
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo,Maji na Mifugo, Said
Nkumba akichangia mada hiyo kwa kuviasa baadhi ya vyombo vya habari
kuacha kuandika habari za kudidimiza viwanda vya haba nchini. Kulia ni
Idd Azzan Mbunge wa Kinondoni na Dunstan Kitandula ambaye ni Makamu
Mwenyekiti was Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara.
Bidhaa mbalimbali zikiwa zimfungwa kwenye viroba
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries
Limited (TDL), David Mgwassa () akifafanua jambo katika semina ya
wajumbe wa Kamati mbili za Bunge za Uchumi,Viwanda na Biashara pamoja
na Kilimo,Maji na Mifugo kuhusu baadhi ya vyombo vya habari vyenye
uhusiano na nchi jirani vinavyotumika kupiga vita viwanda vya ndani
kikiwemo cha Konyagi. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini
Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amos Makala,
akichangia mada katika semina hiyo. Kushoto ni Naibu Waziri wa TAMISEMI,
Kassim Majaliwa na Said Nkumba.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Dunstan Kitandula akichangia mada hiyo.